Hosea 5

Hukumu Dhidi Ya Israeli


1 a“Sikieni hili, enyi makuhani!
Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli!
Sikieni, ee nyumba ya mfalme!
Hukumu hii ni dhidi yenu:
Mmekuwa mtego huko Mispa,
wavu uliotandwa juu ya Tabori.

2 bWaasi wamezidisha sana mauaji.
Mimi nitawatiisha wote.

3 cNinajua yote kuhusu Efraimu,
Israeli hukufichika kwangu.
Efraimu, sasa umegeukia ukahaba,
Israeli amenajisika.


4 d“Matendo yao hayawaachii
kurudi kwa Mungu wao.
Roho ya ukahaba imo ndani ya mioyo yao,
hawamkubali Bwana.

5 eKiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao;
Waisraeli, hata Efraimu,
wanajikwaa katika dhambi zao;
pia Yuda atajikwaa pamoja nao.

6 fWakati wanapokwenda na makundi yao
ya kondoo na ng’ombe
kumtafuta Bwana,
hawatampata;
yeye amejiondoa kutoka kwao.

7 gWao si waaminifu kwa Bwana;
wamezaa watoto haramu.
Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi
zitawaangamiza wao
pamoja na mashamba yao.


8 h“Pigeni tarumbeta huko Gibea,
baragumu huko Rama.
Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni,
Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

ongoza, ee Benyamini.

9 jEfraimu ataachwa ukiwa
katika siku ya kuadhibiwa.
Miongoni mwa makabila ya Israeli
ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia.

10 kViongozi wa Yuda ni kama wale
wanaosogeza mawe ya mpaka.
Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao
kama mafuriko ya maji.

11 lEfraimu ameonewa,
amekanyagwa katika hukumu
kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.

12 mMimi ni kama nondo kwa Efraimu,
na kama uozo kwa watu wa Yuda.


13 n“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,
naye Yuda vidonda vyake,
ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,
na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.
Lakini hawezi kukuponya,
wala hawezi kukuponya vidonda vyako.

14 oKwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,
kama simba mkubwa kwa Yuda.
Nitawararua vipande vipande na kuondoka;
nitawachukua mbali,
na hakuna wa kuwaokoa.

15 pKisha nitarudi mahali pangu
mpaka watakapokubali kosa lao.
Nao watautafuta uso wangu;
katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”
Copyright information for SwhKC